Monday , 6th Apr , 2015

Mashindano ya mchezo wa Judo ya vijana ya Afrika yaliyotakiwa kufanyika June mwaka huu nchini Burundi yamesogezwa mbele mpaka Julai mwaka huu ili kuweza kuzipa timu shiriki nafasi ya kufanya maandalizi kwa ajili ya michuano hiyo.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa Chama cha Judo Tanzania JATA, Innocent Malya amesema mashindano hayo yameipa nafasi timu ya Tanzania pia kwa ajili ya kufanya mazoezi ambapo mpaka sasa vijana waliochaguliwa wanaendelea na mazoezi katika vilabu vyao.

Malya amesema, vijana wanaoendelea na mazoezi ni wale walioshiriki na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika Mashariki na All African Games.