Thursday , 22nd Jan , 2015

MICHUANO ya Judo Kanda ya Tano inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 14 mpaka 15 mwaka huu mjini Moshi kwa kushirikisha nchi sita ambao ni wanachama.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa Chama cha Judo nchini JATA Innocent Malya amesema, nchi shiriki ambazo ni Kenya , Burundi, Rwanda, Zanzibar, Ethiopia na wenyeji Tanzania zitaanza kuwasili mjini Moshi Februari 10 kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo ambapo kutakuwa na semina ya Makocha pamoja na wasimamizi wa michuano hiyo.

Malya amesema, washiriki wa michuano hiyo wanatarajiwa kupima uzito siku moja kabla ya mashindano ambapo wachezaji watakaoanza Februari 14 watapima Februari 13 huku watakaoshiriki Februari 15 wakipima uzito Februari 14.

Malya amesema, timu wenyeji imeshaingia kambini ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano hiyo ambapo kambi zipo makundi mawili na kundi moja lipo Moshi na lingine Dar es salaam.