Sunday , 16th Nov , 2014

Chama cha Judo nchini JATA kimesema kimeamua kuchagua wachezaji wengi wa mchezo huo watakaoingia kambini ili kuweza kuukuza mchezo huo hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa JATA, Innocent Malya amesema timu ya taifa inashirikisha wachezaji watatu kwa kila uzito lakini wanaamini kwa kupitia kambi ya timu ya Taifa wataweza kukuza vipaji vya wachezaji hao.

Malya amesema mpaka sasa wameshapata wachezaji ambao wanaamini wataweza kufanya vizuri katika michuanoya kanda ya Tano ambayo Tanzania itakuwa nchi Mwenyeji wa michuano hiyo.