
Akizungumza na East Africa Radio, Kocha msaidizi wa Klabu hiyo, Boniface Mkwasa amesema, wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo ambayo kwa upande wao ni muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri na kuweza pia kufanya vizuri katika Ligi kuu na kuendelea kushikilia ubingwa.
Kwa upande wa usajili, Mkwasa amesema kunanafasi moja iliyoachwa na mshambuliaji Kpah Sherman aliyesajiliwa na Klabu ya Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini hivyo wapo wachezaji ambao wapo kwenye uangalizi kwa ajili ya kuweza kuziba nafasi hiyo.