
Rashford akishangilia moja ya mabao yake
Manchester United wamedondoka kutoka nafasi ya kwanza msimu uliopita ambapo hawakuwa na matokeo mazuri sana huku Real Madrid ambao walishika nafasi ya pili msimu uliopita wakirudi katika nafasi ya kwanza.
Makamu mwenyekiti wa Manchester United, Ed Woodward aliwahi kusema kwamba muda mwingine matokeo ya uwanjani huwa hayana faida kwenye suala la kibiashara kitu ambacho kimedhihirika sasa kutokana na Man United kuwa na matokeo mazuri chini ya Ole Gunnar Solskjær lakini ikionekana kushuka kwenye suala la mapato.
Real Madrid wametengeneza kiasi cha €750.9m zaidi ya shilingi Trilioni 1.9 huku Barcelona ambao wanashika nafasi ya pili wakitengeneza kiasi cha €690.4m zaidi ya trilioni 1.8. Man United wametengeneza kiasi cha €666m zaidi ya shilingi Trilioni 1.7.
Mapato hayo ni yale yaliyoingizwa katika msimu wa 2017/18 ambapo pia klabu ya Bayern Munich imeshika nafasi ya 4 ikiwa imetengeneza kiasi cha €629.2.
Manchester City wapo nafasi ya 5 wakifuatiwa na PSG wakati Liverpool wakiwa katika nafasi ya 7. Chelsea wapo nafasi ya 8, Arsenal nafasi ya 9 na Tottenham nafasi ya 10.
Ligi kuu ya England imeingiza timu 9 kwenye 20 bora huku Italia ikiingiza klabu 4 ambapo Juventus wameshika nafasi ya 11. La Liga pamoja na Bundesliga zimeingiza timu 3 kila mmoja wakati Ligue 1 ikiingiza timu 2.