
Katika kikosi cha Yanga kilichotolewa muda mfupi uliopita kwajili ya kuivaa Mwadui FC baadae leo, jina la Tambwe limejumuishwa hivyo atakuwa anaongoza safu ya ushambuliaji.
Tambwe ambaye amewahi kuwa mfungaji bora wa Ligi kuu katika misimu miwili tofauti hajaanza vizuri msimu huu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.
Hivi karibuni akiwa kwenye michuano ya Mapinduzi Visiwani Zanzibar, Tambwe alilazimika kurudishwa jijini Dar es salaam kwajili ya kupata matibabu baada ya kusumbuliwa na homa ya Malaria.
Yanga yenye alama 21 katika nafasi ya 5 inashuka kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es salaam kucheza na Mwadui FC inayoshika nafasi ya 11 ikiwa na alama 12. Mchezo huo ni wa raundi ya 13 ligi kuu soka Tanzania Bara.