Wednesday , 2nd Nov , 2016

Serikali imetakiwa kusimamia kwa umakini mchezo wa ngumi hususani ngumi za kulipwa nchini ili kupunguza wimbi la viongozi wa ngumi wanaotumia kigezo cha kusafirisha mabondia ili kupitisha biashara haramu kwenda nje ya nchi.

Waombolezaji wakishusha kutoka kwenye gari jeneza lenye Mwili wa Bondia Thomas Mashali kupeleka eneo la kuagia viwanja vya Leaders dar es Salaam

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga mwili wa bondia wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali, Rais wa Organaizesheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania TPBO Yasin Abdallah 'Ustaadh' amesema serikali inatakiwa kusimamia suala la usafirishaji wa mabondia kwenda nje ya nchi.

Amesema kabla ya kufikwa na umauti bondia huyo alikuwa akichukizwa na baadhi ya watu waliokuwa wakitumia kigezo cha uongozi katika ngumi kwa lengo la kusafirisha mabondia lakini walikuwa wakisafirisha biashara haramu hivyo kupelekea mchezo wa ngumi kudharaulika na kuonekana kama mchezo usio na maadili nchini.

Waombolezaji wakibeba jeneza lenye Mwili wa Bondia Thomas Mashali kupeleka eneo la kuagia katika viwanja vya Leaders

 

Kwa upande wake muandaaji wa mapambano nchini Kaike Siraju amesema, mabondia nchini wanatakiwa kufuata mazuri yote yaliyoachwa na Mashali hususani katika upande wa ngumi ili kuendelea kupandisha kiwango cha ngumi nchini.

Mwili wa bingwa huyo wa zamani wa mataji mbalimbali aliyefariki dunia usiku wa kuamkia juzi baada ya ugomvi uliotokea Kimara Dar es Salaam dhidi ya watu wasiojulikana umeagwa na kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam.

Waombolezaji wakiaga mwili wa Bondia Thomas Masha