
Kocha wa Mbeya City Kinnah Phiri (Kushoto)
Kocha Phiri amesema kuwa kuwa anaamini utakuwa mchezo mzuri na mgumu kwa sababu timu zote mbili zimetoka kushinda mechi zake zilizopita huku akiahidi ‘kuiduwaza’ Yanga kwa kipigo kutokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya kwa kikosi chake na kutupilia mbali hofu yoyote kutoka kwa timu hiyo akiamini timu zote hizi mbili zina mchezo sawa.
Wakati huo huo kiungo wa Mbeya City Fc, Ayoub Semtawa atalazimika kusubiri kwa majuma mawili zaidi kuweza kurejea uwanjani, kufuatia majeraha ya kuchanika nyama za paja mguu wake wa kulia kwenye mchezo dhidi ya African Lyon uliochezwa jijini Dar, wiki moja iliyopita.
Kwa mujibu wa daktari wa kikosi, Dkt. Selaphini Mushi, Semtawa alichanika vibaya nyama za paja baada ya kugongwa na mlinzi wa Lyon wakati alipokuwa akijaribu kukontroo mpira wa juu na kulazimika kutolewa nje kwa msaada baada kushindwa kabisa kutembea kufuatia tukio hilo lililotokea kwenye dakika ya 60 ya mchezo huo.