Thursday , 19th May , 2016

Wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani wanatarajiwa kupata burudani ya mbio za magari, mashindano yanayojulikana kama Alliance Auto MMSC Rally 2016, mwishoni mwa wiki hii.

Mratibu wa mbio hizo Hidaya Kamanga kutoka Mzizima Motor Sports Club, amesema mbio hizo zitaanzia katikati ya jiji na kupitia barabara za Ally Hassan Mwinyi, Bagamoyo, na kumalizikia Magereza Bagamoyo siku ya jumapili.

Sherehe rasmi ya kukabidhi zawadi na vikombe kwa washindi itafanyika Bagamoyo, Mei 22 mwaka huu.