
John Wall na kocha wake, Scott Brook
Imeripotiwa kuwa mchezaji huyo aliingia katika mzozo na kocha wake katika kipindi cha mazoezi huku chanzo chake kikiwa ni pale alipogombana na mchezaji mwenzake Jeff Green, ambapo kocha huyo aliingilia mzozo huo ndipo John Wall alipomtolea lugha za matusi.
Baada ya mzozo huo, John wall aliomba msamaha kwa wachezaji na kocha wake kwa kitendo kilichotokea, lakin mchezaji mwenzake wa kutegemewa Bradley Beal yeye ameuambia uongozi wa Washington Wizard kuwa wamekuwa wanaishi kwenye hali hiyo ya mizozo kwa taktibani miaka saba sasa.
Inasemekana Bradley Beal na John wall ni wachezaji ambao hawapendani kabisa lakin ndio wachezaji wa kutegemewa katika timu hiyo.
Tayari uongozi wa wizard umetangaza kuwauza wachezaji hao kwa timu itakayowahitaji, ukiachana na hao pia wamemuweka sokoni porter junior. Ni ngumu kuwa na kundi la wachezaji wasiopendana kuweza kushinda kwahiyo basi timu ya wizard haina budi kuwauza ili waweze kutengeneza kikosi kitakachoweza kupambana na kuwa na upendo.
Ikumbukwe john wall katika misimu minne tano aliyocheza Wizard amewafikisha katika 'playoffs' mara nne huku uwiano wake wa ufungaji ni alama 20 kwa mchezo mmoja, akitoa 'assists' 7.9 kwa mchezo.