Kikosi cha Yanga
Mchezo huo umesogezwa mbele kwa siku moja kwa sababu Ruvu Shooting imechelewa kutoka Bukoba mkoani Kagera ambako Jumapili iliyopita ilicheza na Kagera Sugar katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limejiridhisha kuwa Ruvu Shooting imechelewa kuingia kituo cha Dar es Salaam, ndiyo maana mchezo dhidi ya Young Africans umesogezwa mbele.
Michezo mingine ya kesho Jumatano inahusisha timu za Mwadui ya Shinyanga na Azam FC itachezwa Uwanja wa Mwadui wakati Simba itasafiri hadi Mbeya kucheza na Tanzania Prisons Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine.
Sababu ya kuvuta nyuma michezo hiyo ni kutoa nafasi ya maandalizi ya kambi ya timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayotarajiwa kusafiri Ijumaa wiki hii kwenda Harare Zimbabwe kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa unaotarajiwa kufanyika Novemba 13, maka huu.








