
Baadhi ya washambuliaji wa Chelsea
Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni katika harakati za klabu hiyo kutafuta dawa ya mshambuliaji akayeweza kusimama kwa mafanikio katika nafasi hiyo inayoonekana kuyumba tangu kuondoka kwa Didier Drogba.
Chelsea imeshuhudia mastraika kadhaa wakipita ndani ya klabu hiyo katika kipindi cha miaka kadhaa ya karibuni ikianzia kwa Fernando Torres ambaye alikuja na moto kutoka Liverpool mwaka 2011 hadi 2015 akicheza mechi 110 na kufunga mabao 20 pekee.
Samuel Eto'o naye aliwahi kupita katika klabu hiyo, akisaini mkataba wa mwaka mmoja msimu wa 2013/14 ambapo alicheza mechi 21 na kufunga mabao 8 pekee ikiwemo hat-trick yake kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Manchester United.
Msimu wa 2015/16 klabu hiyo ilimsajili mshambuliaji, Radamel Falcao kwa mkopo baada ya kutofanya vizuri na Manchester United, ambapo akiwa na Chelsea aliishia kucheza mechi 10 na kufunga bao moja pekee na kuamua kuachana nae.
Diego Costa anaweza kuwa na unafuu kidogo kulinganisha na washambuliaji wengine kwani katika zama zake klabuni hapo alifanikiwa kushinda taji la EPL mara mbili, msimu wa 2014/15 na 2016/17 na katika kila msimu ambao Chelsea ilishinda taji hilo, alifunga mabao yasiyopungua 20.
Msimu wa 2017/18, Chelsea ilijitosa sokoni kwa kutafuta mshambuliaji ambaye atawapa uhakika wa mabao, ndipo walipomnyakua Alvaro Morata kwa pauni milioni 60 kutokea Real Madrid. Mpaka sasa Morata amefanikiwa kucheza mechi 47 klabuni hapo, akiwa amefunga mabao 16 pekee.
Mwezi Januari mwaka uliopita, Chelsea ilimsajili mshambuliaji, Olivier Giroud ili kumuongezea nguvu Morata katika safu ya ushambuliaji ya Chelsea. Ambapo mpaka sasa amecheza jumla ya mechi 31 na kufunga mabao 5.