
Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" Charles Boniface Mkwasa
Afisa Habari wa TFF Alfredy Lucas amesema kuwa Mkwasa atazunguka katika viwanja mbalimbali vya Ligi Kuu na Ligi Daraja la kwanza ili kuweza kuangalia wachezaji wapya watakaounda timu ya Taifa ya Tanzania itakayoshiriki mashindano mbalimbali ya Kimataifa.
Alfredy amesema, programu hiyo itamsaidia Kocha Mkwasa kutokuegemea upande mmoja katika kuchagua wachezaji kwani atakuwa na wachezaji wengi ambao atakuwa akiangalia ni wachezaji gani awachukue katika mashindano mbalimbali.