Monday , 31st Oct , 2016

Andy Murray amebakiza hatua moja pekee ili kuwa kinara wa tenisi duniani, baada ya kumchapa Jo-Wilfried Tsonga kwa seti za 6-3 7-6 (8-6), kwenye fainali ya Erste Bank Open mjini,Vienna.

Andy Murray kushoto akiwa na mchezaji namba moja duniani mchezo wa tenesi Novak Djokovic

 

Mskochi huyo mwenye umri wa miaka 29, anashinda taji la tatu la msimu na ushindi wa saba wa mashindano, na kufikisha pointi 415 nyuma ya Novak Djokovic.

Murray, anaweza kuwa mchezaji namba moja duniani kwa mara ya kwanza endapo atashinda taji la Paris Masters mwezi ujao, na kuombea Djokovic, asifikie fainali ya mashindano hayo.

Wakati huo huo, Dominika Cibulkova amepata ushindi kwa historia ya maisha yake kwa kutwaa taji la WTA baada ya kumchapa mchezaji namba moja duniani kwa upande wa Wanawake, Angelique Kerber kwa seti za 6-3 6-4, huko Singapore.