“Nimeomba (Everton FC) wachukue vijana wawili kwenye vituo vyao vya kukuza soka la vijana, wamelipokea. Nataka kuona miaka michache ijayo tunakuwa na wachezaji wengi katika anga ya kimataifa,” amesema.
Pia Waziri Mwakyembe amesema ataendelea kuikumbusha klabu hiyo mara kwa mara ili kutimiza lengo hilo na kusisitiza kuwa kuna haja ya kuwatafutia wachezaji hao vituo vya soka vya kimataifa wakapate uzoefu wakuze vipaji baada ya kung’ara kwenye michuano ya Afrika nchini Gabon.





