
Kutoka kushoto ni Serena, Naomi katikati na Venus kulia.
Jina la Naomi Osaka lilisambaa na kufahamika na wengi mwaka 2018 alipomfunga kioo chake (Idol) Serena Williams na kuchukua Grand Slam yake ya kwanza kwenye michuano ya wazi ya Marekani.
Akiwa na umri wa miaka 21 tu Naomi amefuzu fainali hiyo kwa kumfunga Karolina Pliskova kwa seti 6-2 4-6 6-4 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa kwa saa moja na dakika 53.
Katika mchezo wa fainali Jumamosi hii atakutana na Petra Kvitova kutoka Jamhuri ya Czech ambaye amefika hatua hiyo kwa kumfunga Mmarekani Danielle Collins 7-6,6-0.
Naomi taratibu anaanza kuzichukua zama za wakali wa mchezo huo kwa wanawake ndugu wawili Serena na Venus Williams. Venus aliishia raundi ya 32 huku Serena alitolewa katika hatua ya robo fainali.