Wednesday , 4th Jun , 2014

Wachezaji wawili waliochaguliwa kwenda nchini Brazil kwenye kambi ya dunia ya Copa Coca-Cola, mapema leo wamekabidhiwa bendera ya Taifa tayari kwa safari hiyo itakayofanyika Jumapili ya June 8 mwaka huu.

Ali Shabani Mabuyu na Juma Yusuf wakikabidhiwa bendera ya taifa na naibu mkurugenzi wa maendeleo ya michezo-wizara ya habari, utamaduni vijana na michezo mama Juliana Matagi Yassoda.

Ali Shabani Mabuyu kutoka Ilala aliyekuwa mchezaji bora wa Copa Coca msimu wa 2013/2014 na Juma Yusuf kutoka Zanzibar aliyeibuka mfungaji bora katika michuano hiyo, wamekabidhiwa bendera ya taifa tayari kwa safari ya Brazil.

Wachezaji hao Ali Shabani Mabuyu kutoka Ilala aliyekuwa mchezaji bora wa Copa Coca msimu wa 2013/2014 na Juma Yusuf kutoka Zanzibar aliyeibuka mfungaji bora katika michuano hiyo, wamekabidhiwa bendera ya taifa na naibu mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mama Juliana Matagi Yassoda katika hoteli ya Kilimanjaro Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Akiongea wakati wa hafla hiyo mama Yassoda alielezea kufurahishwa kwa serikali kutokana na maendeleo ya mchezo huo hapa nchini

Naye Afisa Habari wa mamlaka kuu ya soka Tanzania TFF bwana Boniface Wambura hakusita kuwamwagia sifa vijana hao kutokana na jitihada zao zilizowafikisha hapo.

Awali meneja chapa wa Coca Cola bwana Maurice Njowoka akielezea umuhimu wa kambi hiyo kwa vijana hao alisema vijana hao watafaidika kwani watapata mafunzo kutoka kwa makocha wazoefu.