Mwenyekiti wa Kamati ya usajili, Zakaria Hans Poppe
Hans poppe amebainisha hayo baada ya kuenea kwa tetesi kuwa timu hiyo imeshawasajili wachezaji hao baada ya msimu 2016/2017 kuisha hivi karibuni.
“Ni uongo kusema kuwa sisi tumeshaingia mkataba na mchezaji yoyote maana hadi sasa mikataba ya wachezaji bado haijamalizika, tukisajili mtu sasa itakuja kuwa kama suala la Kessy ambalo tuliwaambia Yanga lakini wakajifanya wajuaji, matokeo yake wametema milioni 50 tena kwa huruma yetu” alisema Poppe.
Pamoja na hayo, Hans poppe amesema kwa sasa hawezi kusema chochote kama wameanza mazungumzo na wachezaji hao wanaotajwa zaidi.






