
Shujaa wa Simba SC inayokwenda hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo ambayo itatoa mwakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mwakani, alikuwa ni mshambuliaji Mganda, Hamisi Friday Kiiza aliyefunga mabao mawili, wakati lingine limefungwa na kinda Hamis Ndemla.
Kiiza alifunga mabao dakika ya 77 kwa shuti kali akimalizia krosi ya Abdi Banda na la tatu dakika ya 90 kwa penalti, baada ya kiungo Said Ndemla kuangushwa kwenye boksi.
Ndemla alifunga bao la pili la Simba SC hii leo dakika ya 90 kwa shuti la umbali wa mita 38, bao lililowasisimua zaidi mashabiki uwanjani, huku bao la tatu likifungwa na Kiiza dakika za nyongeza kwa mkaju wa penati baada ya Ndemla kuchezewa vibaya katika eneo la hatari.
Mapema kipindi cha kwanza, Simba SC ilipoteza nafasi mbili nzuri za mabao, kwanza dakika ya 11 wakati winga Joseph Kimwaga alipowalamba chenga vizuri mabeki wa Burkina Faso, lakini akapiga nje na dakika ya 39 beki Mrundi, Emery Nimubona alipopiga nje akiwa karibu na lango.
Burkina Faso nayo iliyoongozwa na mkongwe, Ulimboka Alfred Mwakingwe aliyewahi kuwika Simba SC ilipoteza nafasi pia.
Dakika ya 39 Ulimboka alimdakisha kipa Muivory Coast wa Simba SC, Vincent Angban shuti dhaifu akiwa kwenye nafasi nzuri na dakika nne baadaye akachelewa kupiga akiwa kwenye boksi kabla ya mpira kuokolewa na mabeki
Katika mechi nyingine za michuano hiyo leo, Toto Africans imeifunga 4-1 Pamba Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, wakati Ndanda FC imeifunga 5-0 Mshikamano Uwanja wa Nagwanda SIjaona mjini Mtwara.
Michuano hiyo itaendelea hapo kesho kwa mechi tatu pia, Yanga SC na Friends Rangers uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Mji Njombe na Prisons Uwanja wa Amaan, Njombe na Stand United na Mwadui FC uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa: Vincent Angban, Hassan Kessy, Abdi Banda, Novaty Lufunga, Jonas Mkude, Emery Nimubona/Mwinyi Kazimoto dk 66, Said Ndemla, Hamisi Kiiza, Mussa Mgosi/Danny Lyanga dk46 na Joseph Kimwaga/Hajji Ugando dk29.
Burkina Faso: Hashim Nzota, Kessy Kessy, Anthony Matangalu, Zawadi Mauya, Hussein Shehe, Victor Mswaki, Sharif Mohammed, Jonathan Kishimba/Jumanne Wida dk69, Ulimboka Mwakingwe na Hassan Mkota/Athumani Mohammed dk46.