
Wachezaji wa Simba na Gor Mahia
Kamati hiyo iliyoketi jana Januari 23, 2019 imesema mchezaji huyo ametimiza vigezo vyote vya kucheza michuano hiyo.
Aidha imefafanua kuwa Lamine amepewa leseni ya muda na shirikisho la soka nchini (TFF) ambayo ni namba 002821M94 hivyo kanuni za michuano zinamruhusu kucheza.
AFC Leopards ambayo ilitolewa jana na Simba kwa kufungwa mabao 2-1 ilikata rufaa kuwa mchezaji huyo ambaye anafanya majaribio Simba hana leseni kucheza michuano hiyo.
Kanuni za mashindano hayo ibara ya 5.5 inataka kila mchezaji anayecheza mashindano hayo awe amepewa leseni kutoka shirikisho la nchi husika.