Emmanuel Okwi na baadhi ya wachezaji wa Uganda
Uganda ambao tayari wameshafuzu fainali hizo zitakazofanyika nchini Misri, wamesisitiza kuwa wanataka kumaliza vizuri wakiwa juu ya kundi L.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa timu ya taifa ya Uganda, (Uganda the Cranes), wameeleza nia yao ya kushinda mchezo wa mwisho. ''Tuonyeshe uwezo wa juu zaidi katika kumaliza hii hatua'', wameandika.
Uganda wameshinda mechi 4 na sare moja katika mechi zao 5 za Kundi L, hivyo kufikisha pointi 14 kileleni huku wakifuatiwa na Lesotho na Tanzania zenye pointi 5 wakati Cape Verde wana pointi 4.
Tanzania inahitaji ushindi ili kufuzu AFCON inayoanza mwezi Juni, lakini itasubiri matokeo ya Cape Verde na Lesotho ambapo inabidi Lesotho ifungwe au kutoa sare.