
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF iliyokutana Jumapili Januari 14,2018 imemfungia mechi 3 Chirwa, ambaye ni kinara wa mabao ndani ya klabu hiyo msimu huu akiwa na mabao saba.
Aidha kamati hiyo imemwadhibu Chirwa baada ya kukiri kosa la kumpiga mchezaji wa Prisons kwenye mchezo wa ligi kuu raundi ya 12 uliopigwa kwenye uwanja wa Azam Complex Novemba 25.
Mbali na kukosa mechi tatu Chirwa pia amepigwa faini ya shilingi laki tano 500,000/=. Chirwa atakosa mchezo wa jumatatno dhidi ya Mwadui FC utakaopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Michezo mingine ambayo Chirwa ataikosa kwa kutumikia adhabu hiyo ni dhidi ya Ruvu Shooting pamoja na mchezo dhidi ya Azam FC.