Monday , 25th Jan , 2016

Kocha mkuu wa klabu ya Manchester United Luis Van Gaal yupo mbioni kutimuliwa kufuatia kuwa na mwenendo mbovu wa kuvuna matokeo mabaya na kikosi chake.

Kwa mujibu wa wa tetezi kutoka vyanzo vya habari nchini Uingereza zinaarifu kuwa kaimu mtendaji wa klabu hiyo Ed Woodward amefanya mazungumzo na wachezaji wandamizi wa klabu hiyo juu ya mbinu za ufundishaji wa kocha huyo zinazoaminika kutoridhisha.

Gazeti la Dail Mail limearifu kuwa Woodward ameshafahamu kuwa wachezaji wa man united hawana furaha kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na wamepoteza imani na kocha wao hali inayopelekea kupoteza mechi ambazo wangeweza kushinda.

Inaaminika kuwa Ryan Giggs huenda akakabishiwa mikoba ya kukinoa kikosi hicho mpaka mwishoni mwa msimu huu huku yeye binafsi akihitaji kuaminiwa na bodi ya klabu na kupewa bajeti na mamlaka ya kusajili wachezaji anaowahitaji.

Dhahma ya kutimuliwa kwa Van Gaal inafuatia kipigo cha jumamosi iliyopita cha bao 1-0 kutoka kwa Southampton wakiwa Old Traford na kuwaacha kwenye nafasi ya Tao pointi 10 nyuma ya vinara Leicester City wenye pointi 47.