Thursday , 30th May , 2019

Baada ya msimu wa ligi kuu soka Tanzania bara 2018/19 kumalizika, klabu mbalimbali zimeanza kusajili kwaajili ya msimu ujao wa 2019/20 huku Yanga wakiwa vinara katika mbio hizo za usajili.

Lamine Moro

Tayari tetesi za kusajili wachezaji mbalimbali zinaendelea kwa upande wa Yanga huku nyota kadhaa wa ndani na kimataifa wakitajwa kumalizana na klabu hiyo.

Kati ya hao yupo beki Lamine Moro kutoka Buildcon F.C. ya Zambia pamoja na Papy Sibomana kutoka Mukura Victory ya Rwanda.

Wengine ni Abdulaziz Makame kutoka Mafunzo ya Zanzibar na Issa Bigirimana kutoka Armée Patriotique Rwandaise ya Rwanda.

Wachezaji wengine ni Ally Mtoni Sonso kutoka Lipuli FC na Mohamed Ally Camara kutoka Guinea.