Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Vita ya Sadick na Mopele kunogesha fainali

Saturday , 18th Aug , 2018

Fainali ya michuano ya Kikapu ya Sprite Bball Kings mwaka 2018, inaanza rasmi leo kwa game 1 kwenye 'best of five' kupigwa kwenye uwanja wa taifa wa ndani ikikutanisha mabingwa watetezi Mchenga Bball Stars dhidi ya Flying Dribblers.

Kushoto ni Baraka Sadick wa Mchenga Bball Stars na kulia ni Baraka Mopele wa Flying Dribblers.

Kuna vitu mbalimbali vya kuvutia kwenye fainali hizo ambapo vita ya pointi inaonekana kuwa kivutio namba moja ikiwa hadi sasa mchezaji Baraka Sadick wa Mchenga Bball Stars anaongoza kwa kufunga pointi nyingi katika tyimu hizi mbili zilizoingia fainali akiwa na jumla ya pointi 100.

Anaye mfuatia kwa karibu ni Baraka Mopele kutoka timu ya Flying Dribblers ambaye mpaka sasa kafunga pointi 92, hivyo wawili hawa watakuwa wanaziongoza timu zao kuelekea kuzipata zile milioni 10 kwa bingwa, milioni 3 kwa mshindi wa pili na kubwa zaidi kwao kama wachezaji ni ile zawadi ya mchezaji bora yaani 'MVP' ambayo ni milioni 2.

Mbali na hilo timu zote zimefanya mabadaliko ya wachezaji ambao walishiriki msimu uliopita, wengine wakiwepo na wengine hawapo. Kwa upande wa Mchenga Bball Stars wao wameongeza sura mpya lakini wengi wamebaki walewale ila wanamkosa Rwehabura Munyagi ambaye ndio alikuwa MVP wa mashindano mwaka 2017. 

Kikosi chao cha msimu  huu kina nyota kama Baraka sadick, Cristian Joseph, Jije Makani, Mgosi Nyameta, Johnson Mohamed, Mohamed Yusuf, Cornelius Mgaza, Ivan Tarimo, Amos Christian na Masero Nyirabu.

Kwa upande wa Flying wao pia wamefanya mabadiliko lakini kikosi chao kimebaki na asilimia kubwa ya wachezaji waliokuwepo msimu uliopita. Mchezaji ambaye wanamkosa uwanjani ni Geofrey Lea lakini wapo naye kwa upande mwingine akiwa kama kocha msaidizi.

Kikosi chao kamili kina wachezaji kama Habirmana Mayeye, Baraka Mopele, Shenta Denis, Elias Samwel, Benedict Kafuru, Mussa Hassan, Steve Mtemihonda, Meddy Makani, Hermes Lazaro na John Mashauri.
 

HABARI ZAIDI

Waziri wa TAMISEMI Mohamed Mchengerwa

Aonya wanaochangia watumishi kutopanda madaraja

Edgar Lungu, Rais wa Zamani Nchini Zambia Akitembea Kuzunguka Mji Mkuu wa Lusaka

Rais wa zamani Zambia Bw. Lungu hatarini kukamatwa

Mkuu wa Ulinzi Ukraine (Picha ya Website)

Zelensky amfukuza kazi mkuu wake wa ulinzi

Baadhi ya Wananchi wa Chindi na Ntinga wakiwa katika Harakati za Kuvuka Mto

Walazimika kulipa hadi 8000 kuvuka mto kwa mtumbwi

Mohamedi Mchengerwa, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Wanaozuia watumishi kupanda vyeo wakaliwa kooni

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma