Monday , 19th May , 2014

Wadau wamesema mpango wa kupeleka wanamchezo nje ya nchi ni wakupongezwa,lakini wataka mpango huo uwe wa kudumu na endelevu kwa michezo yote, pindi kukiwa na michuano mikubwa ya kimataifa mbele yao

Zikiwa zimepita siku chache tangu wanamichezo mbalimbali wa Tanzania waende kwenye mafunzo maalumu ya maandalizi ya michuano ya Jumuiya ya madola itakayofanyika jijini Grascow Scotland, mdau wa michezo ambaye ni nahodha wa zamani wa timu ya mpira wa meza ya Tanzania Ayoub Zuberi, ametoa wito kwa serikali kuendelea na utaratibu huo, hasa tukiwa tunajandaa na michuano mikubwa kama hiyo

Aidha Zuberi amesema kuwa mpango huo uliofanywa na serikali kupitia wizara yake ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wapaswa kupongezwa kwakua utasaidia kuwa na timu imara za michezo mbalimbali ambazo badala ya kwenda kwenye mashindano kushiriki basi zitakua zikienda kushindana na kutwaa medali ama kuibuka na ushindi na hivyo kututoa katika hali ya kuwa vichwa vya wendawazimu kila mchezo tunafungwa ama kupata matokeo mabovu.