Friday , 2nd Sep , 2016

Wadau wa michezo nchini wametakiwa kujitokeza kwa ajili ya kuweza kusaidia vyama mbalimbali vya michezo ili kuweza kushiriki na kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.

Moja ya pambano la mchezo wa mieleka nchini Marekani

Mwenyekiti wa Chama cha Mielekea nchini AWATA Andrew Kapelela amesema, wadau wa michezo wasiangalie mchezo wa aina moja kwani wanatakiwa kujitokeza kuwekeza hususani katika mchezo wa mieleka ili nchi iweze kujitangaza kwa kufanya vizuri katika mashindano makubwa ikiwa ni pamoja na kuwapa vijana fursa ya kuweza kujiajiri kupitia michezo.

Kapelela amesema, vijana wengi wanashindwa kushiriki katika michezo mbalimbali kutokana na wadhamini kushindwa kujitokeza hivyo iwapo wadau watajitokeza kwa wingi na kuwekeza, vijana wataweza kushiriki na hata kuwa na bidii ya kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.