
Akizungumza na East Africa Radio, Sophia amesema, wanapokea mazoezi wanayopewa na yanazidi kuwapa hamasa na kuwaonyesha kuwango chao ili kuweza kufanya mabadiliko zaidi pale wanapoona kunamapungufu.
Sophia amesema, licha ya kukosa mechi nyingi za kirafiki lakini Kocha Kaijage anawajenga kisaikolojia na kila mchezaji anahari ya kujifunza zaidi kile kocha anachofundisha na wanaamini mechi za kirafiki wanazocheza mechi nja wanaume zitazawasaidia kuweza kufika mbali zaidi katika soka.
Sophia amewataka watanzania kuwa na imani kama waliyokuwa nayo kwani wanaweza kufanya vizuri zaidi katika mashindano ya All African Games.