
Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mwa Ligi Kuu baada ya kuifunga Toto Africans ya jijini Mwanza kwa magoli 2-1 uwanja wa CMM Kirumba mwishoni mwa wiki, huku ikiziacha Azam FC na Simba ambazo hapo jana zilitoshana nguvu baada ya kutoka sare ya bila kufungana.
Mara baada ya mchezo huo, Yanga itarejea Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wake wa awali wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola utakaochezwa Mei 07 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.