Thursday , 18th Feb , 2016

Star mwenye umri mdogo katika muziki Young Killer ameanza kuonja ladha ya ndoa kabla ya kufikia hatua hiyo, akiwa anaishi na mpenzi wake Halima kwa muda sasa.

YOUNG KILLER NA HALIMA

Akiongea na E-News Young Killer amesema kuwa, amejipanga kuhalalisha mahusiano yake na mwanadada Halima.

Kwa muda mrefu sasa Young killer na 'girlfriend' wake huyo wamekuwa wakitamba kwa mahaba motomoto katika mitandao ya kijamii wakionekana viwanja mbalimbali.

Young Killer aliongeza kuwa pamoja na kuwa yeye na mpenzi wake wanaonekana kuwa na umri mdogo lakini kwao hawaoni kuwa ni kikwazo kwao kuishi pamoja.