
Hayo yamezungumzwa leo Jijini Dar es Salaam, kwenye mkutano uliowakutanisha Wanajumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa lengo lakuangalia namna gani wameweza kutimiza malengo yao waliyojiwekea katika kukiboresha chama.
Akiongea katika Mkutano huo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Angela Kiziga amesema kuwa lazima vijana kuwa na uvumilivu wa kisiasa, kuwa karibu zaidi na wanasiasa wanaofanya vizuri kujifunza na kuchagua aina ya siasa ambayo haileti chuki kwa jamii.
Akiorodhesha mambo mbalimbali waliyoyafanya kwa ajili ya maendeleo kupitia chama chao alisema ni pamoja na kuchangia damu salama katika mahospitali mbalimbali nchini kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanaohitaji damu hawapotezi maisha kwa kukosa damu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kinondoni Bw. Salum Madenge amesema wameshirikiana na wadau wa maendeleo nchini kwakuhakikisha wanaisaidia serikali katika kusambaza na kutoa huduma muhimu kwa wananchi kama zile za elimu na kutoa misaada kwa vituo vinavyotunza watu wasiojiweza nchini.