Tuesday , 10th May , 2016

Msanii Ommy Dimpoz ambaye anamiliki lebo ya muziki ya Poz kwa Poz (PKP) amesema magumu na changamoto alizozipitia wakati anaanza muziki, ndizo zimemfanya achukue uamuzi wa kusaidia wengine.

Ommy Dimpoz ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha PlanetBongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema pia ilikuwa ndoto yake kuja kusaidia wengine.

' Ilikuwa ni ndoto yangu kusaidia watu wengine, lakini si vibaya kusapoti kipaji ambacho kinaweza kuwa biashara nzuri baadae, mi mwenyewe nimehustle na ndio maana nakumbuka kuwasaidia wenzangu”, alisema Ommy Dimpoz

Pia msanii huyo amezungumzia mahusiano yake mwandani wake ambaye yupo UK kisomea Udaktari, na kusema kwa sasa ameamua kuweka wazi mahusiano hayo kwani tayari amekuwa mtu mzima.

“Nishakuwa mtu mzima ukiweka hivo inapunguza usumbufu, na kwa sasa yeye yupo UK anasomea udaktari”, alisema Ommy Dimpoz