
Bondia wa Tanzania Thomas Mashali amesema kuwa atamtwanga Bondia Sajjad Mehrab wa Iran kwenye pambano la ubingwa wa dunia raundi 12, Mei 14 jumamosi hii kwenye uwanja wa ndani wa Taifa.
Mashali maarufu kama "Simba asiyefugika", amesema ni lazima ampige bondia huyo kutokana na maandalizi makali aliyofanya ili kuliletea sifaTaifa.
Tayari bondia wa Iran, Sajjad Mehrab ameshawasili nchini.