Friday , 25th Apr , 2014

Jukwaa la katiba limemteua Jaji mkuu mstaafu Baranabas Samatta na mhadhiri na mwanaharakati maarufu Afrika Mashariki Prof Patrick Lumumba kuendesha jopo la upatanishi wa pande zinazopingana katika mchakato wa katiba mpya nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba nchini Tanzania Deus Kibamba

Mwenyekiti wa jukwaa hilo Deus Kibamba amesema hatua ya kuwateua wawili hao inatokana na dalili za kukwama kwa mchakato wa katiba mpya, na hata kushindwa kupatikana kwa katiba yenyewe kama ilivyoahidiwa na Serikali kuwa ingepatikana kesho tarehe 26 April 2014.

Kibamba amesema ujuzi na uelewa wa watu hao katika usuluhishi na utatuzi wa migogoro, hususani ile ya kimataifa, utasaidia kupatikana kwa suluhu ya mgogoro unaotishia uhai wa harakati za katiba mpya nchini Tanzania.