
Kikosi cha Yanga
Afisa Habari wa Shirikisho la Soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, Uwanja wa Uhuru ulikuwa katika ukarabati na umeshakamilika katika hatua za awali na Yanga wamechagua uwanja huo kwa ajili ya michezo yao ya nyumbani ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara mara baada ya Serikali kuizuia kutumia Uwanja wa Taifa.
Alfredy amesema, michezo itakayopigwa siku hiyo ni Simba SC watakaokuwa ugenini dhidi ya Mbeya City katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Mwadui akiwa mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Mwadui mjini Shinyanga, Majimaji FC akiikaribisha Kagera Sugar, Mbao FC akicheza dhidi ya Toto African jijini Mwanza, Stand United akiikaribisha Azam FC na JKT Ruvu akiwa mwenyeji wa Tanzania Prisons katika Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani huku Alhamisi Ruvu Shooting akicheza mchezo wake dhidi ya Ndanda kwenye Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.