Tuesday , 11th Oct , 2016

Wiki ya Afrika katika Umoja wa Mataifa imeanza jana ikiwa na maudhui ya kuimarisha ubia kwa ajili ya malengo ya maendeleo endelevu SGDS, utawala bora, amani na utulivu barani Afrika.

Watoto wakiwa kwenye maji

Katika mkutano wa ufunguzi wa wiki ya Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema juhudi zaidi za utatuzi wa migogoro katika ukanda wa nchi za maziwa makuu, ukanda wa Sahel, na maeneo mengine zinahitajika ili kuwezesha maendeleo barani humo.

Kuhusu hali ya kisiasa barani Afrika lakini bado kuna changamoto wakati idadi kubwa ya nchi za Afrika zimeandaa uchaguzi wa vyama vingi, baadhi ya matukio ya ukosefu wa uaminifu yamezitumbukiza katika migogoro.

Akizungumza na idhaa hii muda mfupi kabla ya mkutano huo Kaimu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Muungano wa Afrika AU Erastus Mwencha amesema ili kufanikisha ajenda ya Afrika ya 2063 bara hilo linapaswa kuwa na ajenda moja pekee kwa ajili ya maendeleo endelevu ya bara hilo.