.jpg?itok=BfGLF8lk×tamp=1478025792)
Pikipiki
Mkurugenzi wa Mfuko wa Uwezeshaji Bw. Edwin Chrisant amesema hayo katika mahojiano na Hotmix na kufafanua kuwa hatua hiyo itawasaidia vijana hao kuinuka kiuchumi na hivyo kuachana na utegemezi wa kuendesha pikipiki zinazomilikiwa na watu wengine kitendo ambacho kimewafanya waendelee kupata kipato duni kisichokidhi mahitaji yao ya kimaisha.
Bw. Chrisant amesema tayari programu hiyo imeshaanza kwa majaribio mkoani Ruvuma ambapo vijana kupitia vikundi vyao vya ujasiriamali, wamepatiwa pikipiki zaidi ya thelathini ambazo hivi sasa wanazimiliki na kujiingizia mapato kuliko ilivyokuwa awali.