Tuesday , 27th May , 2014

Msanii D-Malick Dreams kutoka mkoa wa Mwanza ambaye kwa hivi sasa yupo jijini Dar es Salaam amekuja kivingine baada ya kuungana na mkali katika muziki wa bongofleva Mr Blue kwa kutoa kichupa kipya kilichobatizwa jina 'Nilompenda'.

D-Malick au kwa jina kamili Abdulmalick Simbamgeni ameiambia eNewz kuwa hii ni moja ya project yake mpya ambayo imefanyiwa kazi chini ya mkono mahiri wa prodyuza Lamar wa Fishcrab ambaye ndiye anayempa sapoti kwa sasa, huku video ikiongozwa na msanii Benjamin wa Mambo Jambo.

Aidha D-Malick aliyewahi tamba na ngoma zake maarufu za 'Mama mwenye nyumba' na 'Mtima Wange' amesema kuwa hivi sasa anapiga kitabu katika Chuo cha Ustawi wa Jamii, ameomba mashabiki waipokee kazi yake hiyo mpya.

Tags: