Kocha wa Twiga Stars, Sebastaian Nkoma akizungumza na waandishi
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sebastian Nkoma amesema wachezaji 10 kati ya hao wametoka katika Ligi Kuu ya soka ya Wanawake iliyomalizika mapema mwaka huu.
“Nitakuwa na kambi ya siku 12, baadaye nitacheza mchezo mmoja au miwili ya kirafiki Arusha na timu hii naiandaa kwa ajili ya fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika Ghana mwakani,” amesema.





