
Amesema hayo akizindua zoezi la kujiandikisha kupata kitambulisho cha Taifa na kugawa vitambulisho katika Mkoa wa Ruvuma na kukagua zoezi hilo linaendaje kwa mikoa ya Nyanda za Kusini hasa iliyoko mipakani mwa nchi.
Waziri Nchemba amewataka wananchi waache mazoea ya kutafuta kutambuliwa mpaka wanapokuwa na shida hasa za kutaka hati ya kusafiria au migogoro ya ardhi pale anapoambiwa yeye si raia wa Tanzania.
Mh. Nchemba amewagiza viongozi wa wilaya na vijiji kutokuunganisha zoezi la kuandikisha wananchi kupata vitambulisho vya uraia na zoezi lingine lolote akitolea mfano baadhi ya viongozi kuchangisha fedha za kijiji kwa kuwaambia kuwa hutopata kitambulisho mpaka utakapo lipa fedha unazo daiwa na kijiji.