
Rais Magufuli amesema hayo leo baada ya kutembelewa na familia ya Mzee Nguza Viking ilipomtembelea Ikulu kwa ajili ya kutoa shukrani kwa kile alichokifanya Disemba 9, 2017 kwa kutoa msamaha uliowatoa kifunguni walikokuwa wakitumikia kifungo cha maisha.
“Mimi sikutegemea kama mtakuja kuniona na kunishukuru, niliyoyafanya haya si mimi, bali ni mipango ya mwenyezi Mungu, shukurani nyingi zimuendee mwenyezi Mungu aliyetuumba na ndiyo mwenye jukumukubwa la kusamehe, binadamu hatuwezi tukasimama badala ya Mwenyezi Mungu," Rais Magufuli.
Pamoja na hayo Rais Magufuli ameisisitiza familia ya Nguza kuishi maisha mapya ya kumtukuza Mungu kwani maisha yanapita, yana kuanguka, kusimama hivyo wamtegee yeye (Mungu). na kwamba mategemeo yake sasa ni kuona wanafanya kazi na magitaa yananguruma .
Disemba 09, 2017 kwenye sherehe za Muungano wa Tanzania, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 8,158 ikiwemo familia ya Nguza Viking.