Modric anashitakiwa na mamlaka ya mapato ya Hispania kwa kukwepa kodi aliyotakiwa kulipa kutokana na mauzo ya matangazo yenye sura yake kati ya miaka ya 2013 na 2014.
Baada ya kukubali kulipa kiasi hicho cha fedha Modric ameiomba mamlaka hiyo kufuta kesi inayomkabili. Mchezaji huyo amekuwa muhimu kwenye kikosi cha Madrid tangu alipojiunga nayo akitokea Tottenham ya England.
Hata hivyo Modric sio mchezaji wa kwanza kukumbana na kesi hiyo ya kukwepa kodi ambapo nyota wengine wengi wamewahi kushitakiwa. Nyota hao ni Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, kocha Jose Mourinho na Javier Mascherano.






