Monday , 15th Jan , 2018

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania Fortunatusi Musilimu amewataka madereva wote wa magari kuzingatia alama za barabarani hasa katika vivuko vya watembea kwa miguu.

Kamanda Musilimu a,etoa agizo hilo katika ziara ya ukaguzi wa barabara inatoka Mayamaya mkoani Dodoma hadi Mbonga mkoani Manyara, na kusema kuwa watu watakaokiuka sheria za barabarani hasa za kwenye vivuko, watachukuliwa hatua kali za kisheria

Sambamba na hilo Kamanda Musilimu amewataka wananchi kushirikiana kutokomeza ajali za barabarani kwa kutumia namba husika za usalama barabarani, endapo wataona mwendo wa chombo cha usafiri ni hatarishi kwa maisha yao.

Nao wananchi watembea kwa miguu wameomba kuwekewa viashiria vya kuruhusu wao kupita kwenye vivuko vyao ili kuepusha uvukaji wa mtu mmoja.