
Wachezaji wa Man City kushoto na AFC Bournemouth
Kuelekea mchezo huo, zifuatazo ni rekodi za timu hizo mbili ambapo Bournemouth ilipopanda ligi kuu msimu wa 2015/16 ina rekodi mbaya mbele ya mabingwa hao mara 5 wa EPL.
Katika msimu wao wa kwanza kwenye EPL, Bournemouth ilipoteza mechi zote mbili za nyumbani na ugenini. Msimu wa 2015/16 mechi ya kwanza ilichezwa Oktoba 17, 2015 ambapo Man City ilishinda 5-1 nyumbani na mechi ya pili ikapigwa April 2, 2016 ambapo Man City pia ikashinda 4-0 ugenini.
Msimu wa 2016/17, mechi ya kwanza ilichezwa Septemba 17, 2016 na Man City kushinda kwa mabao 4-0 kabla ya mechi ya pili kupigwa Februari 13, 2017 ambapo Bournemouth ilipoteza ikiwa nyumbani kwa mabao 2-0.
Msimu uliopita wa 2017/18 mchezo wa kwanza ulipigwa Agosti 26, 2017 , Bournemouth ikiwa nyumbani ilipoteza 2-1 kisha ikasafiri kwenda Etihad mwezi Desemba 23, 2017 na kupoteza kwa mabao 4-0.
Mechi ya kwanza msimu huu wa 2018/19 inachezwa Jumamosi hii kwenye dimba la Etihad. Je AFC Bournemouth itaondoa uteja kwa Man City? Usikose kutazama 'LIVE' kuanzia saa 11:30 jioni kupitia EATV na TV1.