Friday , 18th Jan , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano amesimulia kwamba anafahamu adha anayoipata mwanamama ambaye ni Mkurugenzi wa TCRA kuwa anatishiwa akidaiwa kwamba yeye ni CHADEMA.

Rais John Pombe Magufuli

Amezungumza hayo leo wakati akishiriki hafla ya makabidhiano ya mfumo mpya wa kusimamia uwazi katika mawasiliano ya simu (TTMS), Makao Makuu ya TCRA, Dar es salaam.

Amesema kwamba afadhali mkurugenzi huyo anayedhaniwa kwamba ni wa CHADEMA, lakini anafanya kazi kwa kuwa anaamini maendeleo hayana chama na anafahamu kwamba hata CCM kuna wezi wengi.

"Mama wewe chapa kazi. Tunataka watanzania wanaochapa kazi bila kujali itikadi ya vyama vyetu. Nataka niwaambie wapo CCM ambao ni majizi kweli, na kila siku anavaa nguo ya kijani lakini ni mwizi kuliko hata wa CHADEMA au wa CUF".

Aidha Rais ameongeza kwamba, "Wizi hauna dini, wachungaji hawa wanatufundisha neno la Mungu mpaka wengine wanalia, lakini unakuta jizi linaenda kutoa sadaka na linabonyea kabisa na linaondoka kimya kimya"