Friday , 17th May , 2019

Jana Mei 16, 2019 mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo, alimalizana na klabu ya Horoya AC ya Guinea kwa dau linalodaiwa kufikia Tsh 230,000,000. Baada ya nyota yake kung'aa sasa msemaji wa Simba Manara amesema beki Yusuf Mlipili atakuwa nyota hivi karibuni.

Kikosi cha Simba

''Mwite Stoper, anavaa jezi namba 'five' iite Tano mgongoni ,Yussuf Mlipili, ni beki imara mno ni akili kubwa iliyochanganyika na nguvu kidogo, halaf ana 'timing' kama za George Masatu'' - amesema Manara.

Manara ameendelea kubainisha kuwa Mlipili hivi karibuni atakuwa beki bora na ghali zaidi Afrika Mashariki.

Mlipili amekuwa mchezaji muhimu kwenye eneo la ulinzi la Simba katika kipindi ambacho beki wao wa kimataifa Pascal Wawa yupo nje ya uwanja kwa majeruhi.

Yussuf Mlipili

Mlinzi huyo alikuwa sehemu ya 'Clean Sheet' waliyopata Simba kwenye ushindi wa magoli 3-0, dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.