Sunday , 1st Sep , 2019

Hospitali ya Taifa Muhimbili imesema majeruhi wawili kati ya 13, waliokuwa wamelazwa katika Hospitali ya hiyo, wamefariki Dunia na kupelekea idadai ya waliofariki kwenye ajali hiyo kufikia 104.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa wa Hospitali hiyo Aminiel Aligaesha amesema waliofariki ni Asha Ally Seleman, na Avelina Pastory Aman.

Amesema kati ya majeruhi 11 waliobaki wanaoendelea kutibiwa hospitalini hapo, sita wapo wodi namba 22 ya Sewahaji na watano ICU.

Ajali hiyo ilitokea Agosti 10, 2019 mkoani Morogoro kwenye barabara ya Morogoro - DSM, baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka na kuwaka moto.