
Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta
Samatta ameyasema hayo leo Alfajiri, kwenye mahojiano maalumu na mtandao wa shirikisho la soka (TFF), alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere.
''Sio kwaajili ya mchezo huu tu dhidi ya Burundi, huwa morali yangu ipo juu tu kila Tanzania inapocheza hata kama mimi nitakuwa sichezi, ila pia uwepo wangu kwenye kikosi huwa naamini naweza kusaidia taifa langu'', ameeleza Samatta.
Nahodha wa Timu ya Taifa @taifastars_ @samagoal77 amewasili kwaajili ya mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar dhidi ya Burundi. Mchezo wa Kwanza utapigwa Burundi Septemba 4 na marudiano Uwanja wa Taifa Septemba 8, 2019. @Tanfootball pic.twitter.com/HaluwkJUus
— East Africa TV (@eastafricatv) September 3, 2019
Tanzania itacheza na Burundi kesho Septemba 4, ikiwa ni mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar. Mchezo wa marudiano utapigwa Uwanja wa Taifa Septemba 8, 2019.
Tayari wachezaji wa timu ya taifa wameondoka nchini, asubuhi ya leo kwa ndege, kuelekea Burundi tayari kwa mchezo huo.