Thursday , 3rd Oct , 2019

Mwanamziki wa Hiphop Moni Centrozone na mpenzi wake Official Nai, wamesema kuwa endapo Mungu akiwajaalia, wanatamani kuwa na idadi ya watoto wengi ili na wao waweze kuijaza Dunia na kwamba idadi ya watoto wanaowahitaji, haitawasumbua katika kuwahudumia kwasababu wamejipanga.

Moni na mpenzi wake Nai

Akizungumza mbele ya kamera za EATV & EA Radio Digital, Official Nai amesema anatamani sana kupata watoto  na atafurahi kama itakuwa hivyo.

"Sina mtoto na wala sijawahi kupata mtoto kwenye maisha yangu,hata Mungu akinijaalia nitafurahi sana kwa sababu napenda watoto, nikipata kama watoto 10, 11, 12 itapendeza zaidi yaani nina mpango wa kuzaa sana na kujaza Dunia" amesema Official Nai.

Nai ameongeza kuwa mtoto aliyekuwa naye kwa sasa ni wa Dada yake, ambaye watu wengi wanajua ni wa kwake, lakini ukweli ni kuwa hajawahi kuzaa na Mwanaume mwingine kama inavyosemekana katika mitandao ya kijamii.