Wednesday , 11th Dec , 2019

Ofisi ya Mkemia Mkuu Kanda ya Kati imepokea sampuli 36 zakupima vinasaba  vyakujua uhalali wa Baba wa watoto (DNA).

Meneja ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kanda ya kati Mussa Kuzumila

Hayo yamebainishwa leo mkoani Dodoma na Meneja ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kati, Mussa Kuzumila wakati akitoa ripoti ya uchunguzi zilizofanyika ndani ya miaka 2.

Meneja ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Kati, Mussa Kuzumila ameongeza kuwa, majibu yao husaidia kumaliza kesi mahakamani kwa wakati. 

Katika hatua nyingine Kuzulima amesema Kanda ya Kati wamepokea kwa wingi sampuli kutoka Jeshi la Polisi za Dawa za Kulevya hasa Bangi na Kokeini, kemikali.